Wapiganaji wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon wametekeleza a wimbi la mashambulizi yaliyoratibiwa siku ya Alhamisi, wakilenga ngome kadhaa za kijeshi za Israel na kusababisha hasara kubwa kwa wanajeshi hao vamizi wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na harakati hiyo ya Muqawama Ijumaa asubuhi, wapiganaji wake walilenga mikusanyiko ya wanajeshi wa Israel pamoja na magari ya kivita katika miji kadhaa ya mpakani ikiwemo Yohmor alShaqif, Rashaf, alQantara na Khiam.

Operesheni hizo zilihusisha mashambulizi makali ya makombora pamoja na vikosi vya ndege zisizo na rubani za mashambulizi ambazo zilipiga mara kwa mara maeneo yaliyokuwa na wanajeshi wa Israel na vifaa vyao vya kijeshi.

Eneo la kihistoria linalozunguka Ngome ya Beaufort lilishuhudia mapigano makali zaidi, ambapo wapiganaji wa Hizbullah walishambulia vituo vya kamandi vya Israel na mikusanyiko ya wanajeshi kwa mawimbi ya mfululizo ya mizinga, makombora mazito na mashambulizi sahihi ya ndege zisizo na rubani.

Hizbullah pia imeripoti kuharibiwa kwa vifaru kadhaa vya kisasa aina ya Merkava katika mashambulizi hayo yaliyolengwa.

Operesheni za Hizbullah zinakuja kama sehemu ya uungaji mkono wake thabiti kwa watu wa Palestina na pia kama jibu la moja kwa moja kwa uchokozi unaoendelea wa utawala wa Kizayuni pamoja na majaribio yake ya kukalia kwa mabavu ardhi ya Lebanon.

Muqawama wa Kiislamu, yaani Hizbullah, umekuwa ukiahidi mara kwa mara kuilinda mamlaka na uhuru wa Lebanon na kuwasukuma nyuma wanajeshi vamizi wa Israel.

Opereshen za hivi karibuni zinaonyesha kuongezeka kwa ufanisi wa mhimili wa muqawama katika kukabiliana na utawala wa Tel Aviv katika nyanja nyingi, na kuyapa jeshi la uvamizi mapigo makali licha ya kuwa na silaha za hali ya juu na nguvu kubwa ya anga.

Vikosi vya uvamizi vya Israel vimekabiliwa na ongezeko la vifo na upotevu wa vifaa vya kijeshi kusini mwa Lebanon huku Hizbullah ikiendelea kuongeza mashinikizo kwa lengo la kubainisha mshikamano na Wapalestina wa Gaza na mapambano mapana ya kikanda dhidi ya sera za kivamizi na kujitanua za Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *