Jeshi la Iran limetangaza kuwa meli kadhaa za kivita za Marekani katika Bahari ya Oman zimelazimika kuondoka katika eneo hilo baada ya vikosi vya Jeshi la Majini la Iran kufyatua risasi za onyo kwa kutumia makombora ya cruise na ndege zisizo na rubani za kisasa.

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, Jeshi la Iran lilitangaza kwamba operesheni hiyo ilikuwa sehemu ya kampeni inayoendelea ya Jamhuri ya Kiislamu ya kukabiliana na “chokochoko za baharini na utekaji nyara wa meli za kibiashara na meli za mafuta unaofanywa na kikosi cha jeshi la kigaidi la Marekani.”

Taarifa hiyo imesema: “Baada ya milio ya onyo kwa kutumia kombora la Qadir na ndege mpya zisizo na rubani za Shahid Dana za Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, manowari za kivita za DDG-103 na DDG-8 ziliondoka mara moja Bahari ya Oman kuelekea Bahari ya Hindi.”

Jeshi la Wanamaji la Iran pia limethibitisha kwamba meli ya kivita ya USS Tripoli—inayobeba helikopta za mashambulizi – pia imelazimika kukimbia Bahari ya Oman.

Kituo cha Udhibiti na Operesheni za Wanamaji cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimetoa onyo kali kwa adui, Marekani na Israel, kikisisitiza umuhimu wa kukomesha mara moja “uharamia na chokochoko za baharini.”

Kimesema ingawa meli za kivita za Marekani sasa zimepita umbali wa makombora yaliyotumika katika operesheni ya onyo, lakini vikosi vya majini vya Iran vina makombora ya masafa marefu ambayo yatatumika bila kusita iwapo italazimu.

Jamhuri ya Kiislamu imesema mara kwa mara kwamba haitavumilia kuingiliwa kijeshi na nchi za kigeni katika maeneo yake huru ya baharini au kuvurugwa usalama na biashara ya kikanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *