Ripoti mpya imefichua nafasi ya mtandao wa satalaiti wa SpaceX wa Starlink katika mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, ikisema teknolojia hiyo inayouzwa kama miundombinu ya raia imekuwa sehemu muhimu ya mashambulizi ya mauaji dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa hivi karibuni wa Reuters, hati za Pentagon na mahojiano na vyanzo vingi yanaonyesha kuwa, mtandao wa satalaiti wa Elon Musk wa Starlink ulitumika kama uti wa mgongo wa operesheni za mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za jeshi la Marekani kwenye vita vya Juni 2025 na Februari 2026 dhidi ya Iran.

Ripoti hiyo imefichua kuwa mtandao huo pia ulitumika kama chombo cha kuyumbisha nchi kisiasa na juhudi zinazoungwa mkono na nchi za Magharibi za kuisambaratisha Jamhuri ya Kiislamu.

Chini ya makubaliano ya 2023, SpaceX inauza toleo mahususi la kijeshi liitwalo Starshield kwa Pentagon. Vituo hivyo vya SpaceX vinaweza kuunganishwa kwenye satalaiti zote za kibiashara za Starlink na nyingine tofauti, ililyo salama zaidi pia inayoitwa Starshield.

Mwanzoni mwa vita, mtandao wa Starlink ulikuwa kipengele muhimu katika mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran. Katika awamu zake za majaribio na utumaji wa makombora, mtandao huo uliunga mkono na kusaidia mifumo mingi, kuanzia ndege zisizo na rubani hadi vyombo vingine vya angani vilivyotumika kwa ajili ya ujasusi wa baharini na mashambulizi ya angani.

Uchunguzi wa Reuters unathibitisha kwamba kampunii ya Starlink ilitoa picha mubashara za video na mwongozo kwa mabomu yaliyokuwa yakirushwa kutoka kwenye ndege isiyo na rubani aina ya LUCAS iliyotengenezwa kwa kuiga na kufanya uhandisi kinyume (reverse-engineered) wa ndege maarufu isiyo na rubani ya Iran, aina ya Shahed.

Maelfu ya vituo vya Starlink vilivyoingizwa Iran kimagendo pia vilisaidia matumizi rasmi ya kijeshi.

Kwa mujibu wa The Wall Street Journal, Marekani iliingiza takriban vituo 6,000 vya Starlink nchini Iran kwa siri mnamo Januari 2026 pekee. Sehemu kubwa ya manunuzi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ya karibu vituo 7,000 vya Starlink mwezi Januari mwaka huu ilitumia fedha zilizotengwa kutoka “mipango kama hiyo eti ya uhuru wa intaneti” ili “kusaidia wale wanaodaiwa kuwa wanaharakati wanaopinga utawala, kuepuka kufungiwa intaneti nchini Iran”.

Inakadiriwa kuwa kati ya vituo 30,000 na 50,000 vya Starlink vimeingizwa nchini Iran kimagendo tangu mwaka wa 2022.

Serikali ya Marekani ilishiriki moja kwa moja na kwa makusudi katika mpango huo, na Rais Donald Trump alikuwa na habari kuhusu ulanguzi wa teknolojia hiyo ya matumizi ya aina mbili, ambayo ilikuwa ikiongoza ndege hatari zisizo na rubani kuingia katika anga ya Iran.

Usafirishaji haramu huo ulitangazwa na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi kuwa ni juhudi za kuunga mkono “Uhuru wa Intaneti”.

Mamlaka ya Iran yalitwaa vifaa hivyo na kusambaza zana za kuzuia mawasiliano katika miji mikubwa ili kuvuruga mawasiliano hayo. Wizara ya Upelelezi ya Iran pia ilionya kwamba vituo vya Starlink vilikuwa vikitumika kwa ajili ya “ujasusi wa kielektroniki na hujuma,” na kwamba ni “bidhaa za kuvuruga usalama”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *