#HABARI: Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Lazeck Kyamba, ameongoza operesheni maalum ya kuondoa malori yaliyokuwa yameegeshwa kinyume na taratibu katika eneo la Mbagala Zakhem.
Mhandisi Kyamba ameeleza kuwa kuongezeka kwa shughuli za usafirishaji kumesababisha idadi kubwa ya malori kusimama katika eneo hilo, hali inayochangia msongamano mkubwa wa magari na kuhatarisha usalama.
Amebainisha kuwa baadhi ya madereva wamekuwa wakiegesha holela kwenye barabara saidizi (service road), jambo linaloathiri miundombinu na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wengine wa barabara.
Katika operesheni hiyo, TANROADS imetoa elimu kwa madereva kuhusu umuhimu wa kutumia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya maegesho ya magari makubwa na kuwahimiza kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Mhandisi Kyamba amesisitiza kuwa doria na operesheni hizo zitaendelea kufanyika mara kwa mara ili kuhakikisha nidhamu ya matumizi ya barabara inarejea.
Alimalizia kwa kuwaomba madereva wote kushirikiana na mamlaka husika kwa kufuata maelekezo ili kuhakikisha miundombinu hiyo inatumika kwa usalama, ufanisi, na kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na serikali.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)