‎#HABARI: Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Reuben Kwagilwa, ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Bonde la Wami/Ruvu, pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kufanya upya mapitio ya vibali vya usafishaji wa Mto Msimbazi ili kuzuia uharibifu wa mazingira.

Mhe. Kwagilwa ametoa agizo hilo akiwa katika daraja la Kinyerezi kufuatia malalamiko ya wananchi kuwa shughuli za usafishaji mto huo zimegeuka kuwa uchimbaji holela wa mchanga unaochochea mmomonyoko wa ardhi.

Alisisitiza kuwa Serikali haitavumilia kuona uwekezaji wa mabilioni ya fedha katika miundombinu ya umma unaharibiwa kwa matumizi yasiyo sahihi ya vibali hivyo.

Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri ameelekeza taasisi zote zinazohusika kutembelea maeneo yote yaliyopewa vibali ili kujionea hali halisi na kufanya tathmini ya kina ya kimazingira.

Alikumbusha kuwa lengo kuu la vibali vya usafishaji wa mito ni kulinda mazingira na kuboresha mtiririko wa maji, na si kufanya biashara ya mchanga.

Amewataka wataalamu wa mazingira, mamlaka za mabonde, na halmashauri kushirikiana kwa pamoja katika mapitio hayo, akifafanua kuwa uharibifu huo ukiachiwa uendelee utaleta athari kubwa na kuifanya mifumo ya usimamizi kuonekana hovyo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *