#HABARI: Wananchi mkoani Mtwara wameaswa kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili kuruhusu ukuaji wa kasi wa kiuchumi, uwekezaji wa viwanda, na shughuli zingine za kimaendeleo.
Wito huo umetolewa na watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, ambapo walishirikiana kufanya usafi kwenye chanzo cha maji cha Mchuchu kilichopo Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Watumishi hao walibainisha kuwa Mtwara inakua kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa wageni na kasi kubwa ya ujenzi wa viwanda, jambo linalofanya utunzaji wa vyanzo hivyo kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo endelevu.
Kwa upande wake, Meneja wa Usimamizi wa Mazingira na Uratibu wa Jumuiya za Watumia Maji katika bodi hiyo, Batuli Seif, amewasihi wananchi kulinda maeneo ya vyanzo vya maji kwa kupanda miti ili kuhifadhi uoto wa asili.
Alisisitiza kuwa uhifadhi huo ni muhimu kwa usalama wa rasilimali hiyo sasa na kwa faida ya vizazi vijavyo. Aliongeza kuwa jamii inapaswa kuwa walinzi wa kwanza wa vyanzo hivyo ili kuepuka uhaba wa maji unaoweza kukwamisha ustawi wa jamii na shughuli za kiuchumi mkoani humo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)