‎#HABARI: Kampuni tanzu ya TANESCO ya kuzalisha nguzo za zege (TCPM) imeanza rasmi kusambaza nguzo za zege zilizozalishwa katika kiwanda chake kipya mkoani Tabora ili kuimarisha miundombinu ya usambazaji wa umeme nchini.

Kaimu Meneja Mkuu wa TCPM, Mha. Khadija Abdallahmed, ameeleza kuwa nguzo hizo zimeanza kusambazwa mkoani Tabora na mikoa jirani, huku akishukuru Serikali na TANESCO kwa uwezesha wa kiwanda hicho.

Nguzo hizi za zege zina uwezo wa kudumu kati ya miaka 50 hadi 100, hatua itakayosaidia kupunguza changamoto za kukatika kwa umeme zilizokuwa zinasababishwa na nguzo za miti kuoza, kuanguka, au kuungua moto.

Kwa upande wake, Meneja wa Usanifu na Ubora wa TCPM, Mha. Emmanuel Mrema, amefafanua kuwa nguzo hizo zimeleta maboresho makubwa ya kiusalama kwa kuwekewa mfumo wa ‘’earth wire’’ ndani ya nguzo yenyewe.

Tofauti na hapo awali ambapo waya huo uliwekwa nje na kuchochea wizi pamoja na kuhatarisha miundombinu ya TANESCO, muundo huu mpya unamaliza kabisa uhalifu huo.

Kiwanda hicho kimekuwa suluhisho la kisasa linalohakikisha ubora wa hali ya juu na usalama wa kudumu katika gridi ya taifa.

Kiwanda hiki kinachosimamiwa na TCPM kilijengwa mwaka 2024 na kukamilika rasmi mwezi Februari 2026 kwa gharama ya shilingi bilioni 7.9 zilizofanikisha ujenzi na uzalishaji wake.

Hadi sasa, tayari kimefanikiwa kuzalisha jumla ya nguzo za zege 1,195 ambazo ziko tayari kusambazwa kwa wateja katika maeneo mbalimbali nchini.

Kuanza kwa usambazaji huo mnamo Juni 4, 2026, kunadhihirisha mafanikio makubwa ya uwekezaji huo uliolenga kuleta mapinduzi ya nishati nchini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *