Meja Jenerali Mohsen Rezaei Mshauri wa Masuala ya Kijeshi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa Rais Donald Trump wa Marekani amesimamisha mazungumzo kati ya Tehran na Washington, na kuonya kuwa ikiwa vita vingine vitaanza, wigo wake utaenea kutoka Bahari ya Hindi hadi Bahari ya Shamu na Mediterania.

Rezaei ambaye pia alikuwa Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wakati wa vita vya kulazimishwa vya miaka minane katika muongo wa 1980 kati ya Iran na utawala wa Baathi wa Iraq uliong’olewa madarakani, ameeleza haya katika mahojiano maalumu na Fred Pleitgen, ripota wa CNN mjini Tehran.

Marekani na Israel ziliishambulia Iran mwishoni mwa Februari mwaka huu na kumuuwa shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na makamanda kadhaa wa ngazi ya juu wa jeshi. 

Iran ilijibu mapigo kwa mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya ngome na kambi za kijeshi za Israel na pia kushambulia maslahi ya Marekani katika Ghuba ya Uajemi.

Meja Jenerali Mohsen Rezaei ameitahadharisha Marekani kuhusu kuanzisha tena mzozo na kueleza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu itapanua vita nje ya Ghuba ya Uajemi, itapanua oparesheni za kijeshi kutoka Mlango Bahari wa Hormuz hadi Bahari ya Hindi, Mlango Bahari wa Babul Mandab, Bahari Nyekundu na Mediterania.

Amesema mpira upo katika uwanja wa Trump na kwamba Marekani inapasa kuziachia mali za Iran zinazozuiwa kama hatua ya kujenga uaminifu mkabala wa makubaliano yoyote yanayoweza kufikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *