Kocha wa soka wa Iran na mchezaji wa zamani wa kimataifa ameishutumu serikali ya Marekani kwa kuingiza siasa katika michezo, akitaja vikwazo vya visa na matatizo ya kiutawala yanayowakabili wachezaji na wasimamizi wa Timu ya Taifa ya Soka ya Iran.

Akizungumza na tovuti ya Press TV siku chache kabla ya Kombe la Dunia la 2026, Farzad Ashoubi , aliyewahi kuichezea timu ya taifa ya Iran na ambaye sasa anafundisha klabu ya ndani, amesema masharti ya visa ambayo yanalazimisha timu ya taifa ya Iran kuingia Marekani, kucheza mechi, na kuondoka ndani ya siku hiyo hiyo ni “jambo la kushangaza na lenye matokeo mabaya.”

Amesema hatua hizo zinaibua maswali mazito kuhusu uwezo wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, na uwezo wake wa kuhakikisha mazingira ya ushindani yaliyo sawa kwa nchi zote zitakazoshiriki katika tukio kubwa zaidi la michezo duniani.

Ashoubi amesema FIFA  imeshindwa katika majukumu yake  huku kielezea mipango ya mwaka huu  kuwa “ni janga.”

Ameongeza kuwa mazingira ambayo Timu ya Taifa ya Iran italazimika kushindana katika Kombe la Dunia la FIFA 2026 ni “ya kipuuzi na ambayo kimsingi ya haki.”

Siku ya Jumamosi, balozi wa Iran nchini Mexico, Abolfazl Pasandideh, alithibitisha kwamba visa vilivyotolewa kwa wachezaji wa Iran vina sharti la kuingia na kutoka Marekani ndani ya siku moja.

Kwa Ashoubi, ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Timi ya Taifa ya Soka ya Iran maarufu kama Team Melli, athari za masharti hayo ni kubwa.

“Je, timu inaweza kweli kusafiri kwa ndege kwa saa tatu siku ya mechi, iingie uwanjani mara moja, halafu itarajiwe kutoa kiwango bora cha mchezo?” alihoji. “Ni lazima turuhusiwe kulala katika jiji la mechi usiku mmoja kabla ili kukabili siku ya mechi kwa utulivu na kujiamini.”

Masharti ya visa pia yanaongeza ugumu kwa timu ya Iran, ambayo tayari inakabiliwa na changamoto nyingine. Marekani , ambayo ni mwenyeji mwenza wa mashindano hayo pamoja na Canada na Mexico , imekataa kuwaruhusu maafisa wa usimamizi wa timu hiyo.

Miongoni mwa wanaoripotiwa kukataliwa visa ni meneja wa timu Mehdi Mohammadnabi, katibu mkuu wa Shirikisho la Soka la Iran Hedayat Mombeini, pamoja na wakuu wa idara za vyombo vya habari, wachambuzi wa kiufundi na afisa wa mahusiano ya kimataifa ya soka la Iran.

Rais wa Shirikisho la Soka la Iran, Mehdi Taj, naye anaripotiwa kunyimwa ruhusa ya kuingia.

Katika taarifa kali iliyotolewa Jumamosi, shirikisho la soka la Iran lilisema hatua hiyo ni “ukiukaji wa wazi wa kanuni za kimataifa za michezo,” na kwamba Washington imeunda “mazingira ya kibaguzi na yasiyo ya usawa.”

Shirikisho hilo liliongeza kuwa hatua hiyo ni “kuingizwa kwa siasa katika michezo kwa namna mbaya zaidi.”

Iran imepangwa kuanza kampeni yake ya Kombe la Dunia kwa kucheza dhidi ya New Zealand mjini Los Angeles tarehe 15 Juni, kabla ya kukutana na Belgium mjini Los Angeles na baadaye Egypt mjini Seattle , mechi zote tatu zikifanyika nchini Marekani.

Mjadala huo umejitokeza katika mazingira ya mvutano mpana uliosababishwa na vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran. Vita hivyo haramu vimesababisha kuvurugika kwa mashindano ya soka ndani ya nchi na kulazimisha timu ya taifa kujiandaa kwa mashindano hayo nchini Uturuki na Mexico.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *