Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuokotwa kwa miili ya watu sita katika Mto Ruvu, likisema tukio hilo si la kweli na ni taarifa ya uongo iliyozushwa tangu mwaka 2016.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi Salim Morcase, taarifa hiyo imekuwa ikijirudia kusambazwa katika mitandao ya kijamii licha ya kutolewa ufafanuzi mara kadhaa.

Amesema kwa mara ya kwanza taarifa hiyo ilisambazwa Desemba 2016 na kufanyiwa ufafanuzi, kisha ikasambaa tena mwaka 2025 na kutolewa ufafanuzi mwingine, lakini imeendelea kuibuka upya mwaka 2026.

Kamanda Morcase amewataka wananchi kupuuza taarifa hizo na kuacha kuzisambaza, akionya kuwa zinaweza kusababisha taharuki isiyo ya lazima katika jamii.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia chanzo cha taarifa hizo, na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika watakaobainika.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *