Polisi nchini Afrika Kusini wanawatafuta watu waliowapiga risasi na kuwauwa watu 12 jijini Johannesburg siku ya Jumanne.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Watu 10 waliokuwa na silaha wanashukiwa kutekeleza mauaji hayo katika mtaa wa Cleveland, Jumanne usiku, na baadaye kukimbilia kwenye gari jeupe.

Polisi wameelezea tukio hilo kama la kinyama, lililowaacha watu wengine tisa wakiwa na majeraha.

Uchunguzi wa awali unaeleza kuwa huenda mauaji hayo yametokana na tofauti kati ya makundi yanayohusika na uchimbaji wa madini ya dhahabu jijini Johannesburg.

Matukio ya uchimbaji wa madini haramu  nchini Afrika Kusini ni ya kawaida, lakini pia matukio ya watu kushambliwa kwa silaha, yameendelea kushuhudiwa mara kwa mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *