
Jeshi la Iran limetangaza usiku wa Jumatano Juni 10, kuamkia Alhamisi, Juni 11, kwamba sasa litalenga meli yoyote inayopita Mlango-Bahari wa Hormuz. Kwa upande wake, jeshi la wanamaji la nchi hiyo limesema kwamba limeshambulia meli mbili zilizokuwa zikijaribu kuvuka njia ya maji ya kimkakati. Matangazo haya mawili yamekuja muda mfupi baada ya mashambulizi mapya ya Marekani dhidi ya Iran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jeshi la Iran limetangaza kulenga meli yoyote inayopita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz, huku jeshi la majini la nchi hiyo likisema kuwa limeshambulia meli mbili zilizokuwa zinajaribu kupita kwenye njia hii ya maji ya kimkakati.
“Meli yoyote inayopita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz itatakiona cha mtima kuni,” makao makuu ya jeshi la Iran ikinukuliwa na shirika la habari la Tasnim, imetangaza na kuongeza kuwa njia-bahari sasa “imefungwa kabisa kwa aina zote za meli” kufuatia mashambulizi mapya ya anga ya Marekani dhidi ya Iran.
Jeshi la majini la Iran, lililonukuliwa na televisheni ya serikali ya IRIB na shirika la habari la Mehr, limedai kuwa “meli mbili zilizokuwa zikijaribu kupita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz kinyume cha sheria zilishambuliwa.”