Uganda imeshtumu vikwazo vya safari ya angaa vilivyowekwa na mataifa kadhaa ikiwemo Marekani, kufuatia maambukizi ya virusi vya Ebola, ambavyo vimeingia nchini humo kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katibu katika Wizara ya afya nchini Uganda, Diana Atwine, pamoja na mamlaka ya safari za angaa nchini humo na mabalozi, wanasema tangazo la mataifa hayo kuzuia safari za ndege nchini Uganda ni uonevu.

Mbali na Marekani, Canada na Falme za Kiarabu ni miongoni mwa mataifa ambayo yametangaza kusitisha safari za ndege nchini Uganda kwa sababu ya virusi vya Ebola.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus akiwa jijini Kampala wiki hii, alipongeza namna Uganda inavyopambana na Ebola na kuongeza kuwa, kufungwa kwa mipaka sio suluhu ya kupambana na virusi hivyo.

Mpaka sasa Uganda imethibitisha maambukizi ya Ebola 19, ikiwemo vifo viwili, wote kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waliokuwa wamekuja nchini humo.

Mpaka sasa virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo, havina dawa au chanjo ya kupambana na maambukizi hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *