Marekani na Iran huenda zikatia saini mkataba wa kusitisha vita, ndani ya saa 24 zijazo, kwa mujibu wa Pakistan, ambayo ni mpatanishi wa mzozo huu wa Mashariki ya Kati.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif, amesema pande zote zinaelekea kuelewana kwenye masuala tata na kuna matumaini makubwa ya mwafaka kupatikana.

Tangu kusitishwa kwa vita tarehe nane mwezi Aprili, kumekuwa na mazungumzo kati ya Marekani na Iran chini ya Pakistan lakini hakujawa na makubaliano yeyote.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Sharif, amesema makubaliano yanakaribia sana kufikiwa kati ya pande zote ambazo zinatarajiwa kutiwa saini.

Kauli hii inakuja baada ya Waziri wa Mambo ya  nje wa Iran Abbas Araghchi kuandika kwenye mitandao yake ya kijamii, kwamba hakuna matumaini ya mkataba huo kupatikana hivi karibuni.

Katika hatua nyingine, msemaji wa Wiazara ya Mambo ya nje wa Iran ‌Esmaeil Baghaei, amesema kuna uwekezano wa mkataba huo kutiwa saini siku ya Jumapili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *