
Canada. Kuna jamii nyingi zenye mila za ajabu na ovyo. Leo, tutadurusu jamii zenye mila mbovu za ndugu kwa ndugu kurukiana hata nyingine kuoana kwa sababu na visingizio mbalimbali.
Katika kudurusu mila za ndugu kwa ndugu kuwa na uhusiano kingono hata kuoana, kuna baadhi ya visababishi. Mojawapo ya visababishi hivi ni eti kuepuka mali kwenda mbali!
Tunadhani wanaofanya hivi kuna athari hasi wasizojua. Mfano, utafiti umegundua kuwa kwenye ndoa hizi ambazo kwa Kiingereza huitwa endogamy, wahusika wana uwezo mkubwa wa kuzaa watoto mataahira au walemavu.
Mtaalamu wa Australia aitwaye Gregoire Mendes alifanya utafiti wa vinasaba ya urithi na kuja na kile kiitwacho Mendelian law inayoonya kuhusu athari za ndugu kuzaliana.
Wenye kuoana ndugu kwa ndugu wajue kabisa kuwa, panapokuwapo magonjwa ya kurithi, wahusika wajue janga wanalotengeneza. Ndiyo maana utaona jamii zinaozoozesha ndugu kwa ndugu zina watoto wenye ulemavu.
Kwa vile wengi hawajui hili, utasikia kuwa huyu alichezewa eti kulinda utajiri. Hakuna cha utajiri bali mila mbovu na ujinga.
Sababu nyingine ni uzinzi wa kawaida. Utakuta kila mwanaume ajaye kuwatembelea anaitwa anko. Ukiuliza vipi, hakuna majibu yanayaoingia akilini.
Uzinzi na tamaa za kingono, kimsingi, ndizo sababu kubwa za wahusika kujamiiana ndugu. Wapo wanaojua udhaifu huu ambao hawaoi kabisa kwenye makabila yao.
Kihistoria, jamii, kama vile Waarabu huoana ndugu kwa ndugu. Utamaduni unaenda mbali sana. Hapo zamani, makabila ya Kiarabu yalikuwa na uhasama kiasi cha kila kabila hata koo kujikuta imezungukwa na maadui kiasi cha kuoleana ili kuepuka kuoa au kuolewa na adui.
Sababu nyingine ya ndoa za watu wenye uhusiano wa damu ni dini. Kuna dini hasa za kigeni au kimapokeo zinaharamisha ndoa baina ya watu wa dini tofauti.
Hii nayo ni sababu mojawapo ya ndugu kuoana wasijue kuwa wanachofanya kinaweza kuwa hatari kwa watoto wao.
Kwa vile jamii za sasa zimeelimika na zina uhuru wa kutosha, makatazo kama haya hayana msingi. Na isitoshe, mapenzi huwa hayachagui na ni suala la mtu binafsi. Hivyo, hapaswi mtu mwingine au taasisi kumuamria mtu nani wa kuoa au kuolewa naye.
Pamoja na makatazo ya kidini, dini au jamii zenye makatazo haya zina aina fulani ya ubaguzi uwe wa dini au rangi. Mfano, kuna baadhi ya jamii za kigeni zilizolowea Afrika ambazo wanaume wake hupenda kuoa mabinti wa jamii zilizowapokea lakini hawako tayari kuwaoza mabinti zao kwa wanaume wa jamii hizi.
Kwa wazaliwa na wakazi wa mwambao, wanajua fika tunachoongelea. Unaweza kufanya utafiti wako mwenyewe kwa majirani zako kutoka jamii husika ambazo hatutazitaja.
Wakati wa sera za kibaguzi kule Marekani, wanaume wa kizungu walizaa na wanawake wa Kiafrika na wale wa jamii za asili za bara la Amerika lakini kulikuwapo visa vya wamilki wa watumwa kuwabaka watumwa wa kike na kuwapa mimba.
Wakati wamiliki wa watumwa waliokuwa wanaume wakiwabaka watumwa wa kike, wanawake wa kizungu tena waliokuwa kwenye ndoa nao walianza kufanya uzinzi na wanaume wa kiafrika hasa watumwa huru.
Haya yalifichuliwa na msomi Marie S. Molloy kwenye andiko lake la mwaka 2024 lenye kichwa cha habari White, Female Adultery across the Color Line in North Carolina during Slavery and Reconstruction, c. 1800–1870.
Pamoja na ubaguzi kupigwa marufuku nchini Marekani, kuna ushahidi mwingi kuwa wanawake wa kizungu huvutiwa sana na maumbo ya wanaume wa Kiafrika.
Katika andiko lake Angel Wallis anaaandika “Wanawake weupe wengi hupata nguvu, kujiamini, na swag hubamba kivyake. Unaingia chumbani na mwanaume mweusi, boom, unausikia mvuto.”
Wakati wanawake wa kizungu wakivutiwa na Waswahili, kwa Waasia ni kama mwiko kwa binti kuwa na mume mweusi, japo siku hizi, wameanza kubadilika.