Shambulio lililofanywa na wanajihadi, wanaoshukiwa kuwa wa kundi lililolengwa na mashambulizi ya anga ya Marekani mwezi Desemba mwaka uliyopita, limesababisha vifo vya watu 20 kaskazini magharibi mwa Nigeria, kulingana na ripoti ya usalama iliyotolewa siku ya Jumapili, Juni 14.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Makundi ya wanajihadi na magenge ya wahalifu, wanaojulikana kama “majambazi” na wakazi wa eneo hilo, wanajulikana kwa utekaji nyara kwa ajili ya fidia na wizi wa ng’ombe, kutisha jamii kaskazini na katikati mwa Nigeria. Wanafanya mashambulizi mabaya na kuwatoza kodi wakulima wanaotafuta njia ya kuingia katika mashamba yao.

Ripoti ya usalama inayoelezea shambulio hilo, iliyoandaliwa  na kuandikwa kwa ajili ya kuwasilishwa kwa Umoja wa Mataifa na kupitiwa na shirika la habari la AFP, inaonyesha kwamba wanajihadi, wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Lakurawa, walifanya mashamulizi katika jamii ya Fesken Rafi katika wilaya ya Arewa ya Jimbo la Kebbi, karibu na mpaka na Niger, “yaliyosababisha vifo ya zaidi ya watu 20.” Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, mashambulizi hayo yalifanyika siku kadhaa zilizopita lakini yaliripotiwa mwishoni mwa wiki iliyopita tu, kufuatia ziara ya naibu gavana wa Jimbo la Kebbi katika eneo hilo.

Ripoti inasema shambulio hilo lilitokea baada ya utulivu wa ghasia za Lakurawa katika miezi ya hivi karibuni.

Lakurawa imeendelea kuendesha harakati zake kando ya mpaka kati ya Nigeria na Niger, licha ya juhudi za vikosi vya usalama kuwafukuza kutoka Kebbi.

Ripoti hiyo inaonya kwamba ghasia za kundi hili la wanajihadi zinaweza kuongezeka na kuwa “tishio la kimataifa” kutokana na muundo wake wa kimataifa, na kuzidisha juhudi za kupambana na ugaidi.

Baadhi ya watafiti wanaweka uhusiano kati ya Lakurawa na Islamic State huko Sahel (IS), ambalo linafanya kazi hasa nchini Mali na nchi jirani ya Niger.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *