K#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema kuwa ndani ya siku 14 ofisi yake itatoa majibu rasmi kuhusu sakata la kuvunjwa kwa mageti ya ulinzi katika eneo la Upanga, linalomilikiwa na National Housing Corporation (NHC), Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo na kujionea hali halisi ya tukio, DC Mpogolo amesema serikali imepokea malalamiko ya wananchi na kuanza mchakato wa uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira yote yaliyopelekea kuvunjwa kwa mageti hayo pamoja na wahusika wa tukio hilo.

Sakata hilo limeibuka siku chache baada ya wakazi wa eneo hilo kudai kuwa watu waliotambulika kama mabaunsa walifika na kuvunja mageti hayo wakidai kutumwa na uongozi wa mtaa.

Kutokana na malalamiko hayo, Mkuu huyo wa Wilaya amesema hakuna upande utakaohukumiwa kabla ya uchunguzi kukamilika na kusisitiza kuwa serikali itazingatia sheria, haki na maslahi ya wananchi katika kufikia maamuzi ya mwisho.

“Tumefika hapa kujionea wenyewe hali ilivyo na tumeelekeza uchunguzi ufanyike. Ndani ya siku 14 tutatoa majibu rasmi kuhusu suala hili,” alisema Mpogolo.

Wananchi wa eneo hilo wameiomba serikali kuhakikisha uchunguzi huo unafanyika kwa uwazi na haki ili kubaini ukweli wa tukio hilo na kurejesha utulivu katika eneo husika.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *