Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Maji ya Chai kwa tuhuma za mauaji ya Husna Shabani mkazi wa Majengo Jijini Arusha na kisha kutupa mwili huo katika chemba ya maji taka.
Akitoa taarifa hiyo leo Juni 15, 2026 Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema mtuhumiwa alimjeruhi mhanga sehemu mbalimbali za mwili wake ambayo yamechangia kupoteza uhai kwa mwanamke huyo
Masejo ameeleza kuwa uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo umebaini kuwa kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa na marehemu walikuwa pamoja kwenye starehe katika eneo hilo, huku akibainisha wanakamilisha uchunguzi kwa taratibu nyingine za kisheria.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuheshimu utu na uhai wa wengine, kwa kutatua migogoro kwa njia za amani na kutoa taarifa za uhalifu ili kuimarisha usalama na amani katika jamii.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)