Chanzo cha picha, Getty Images
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 1
Arsenal wameripotiwa kuanza mazungumzo ya kumsajili kiungo Ayyoub Bouaddi, mwenye umri wa miaka 18, ambaye aliisaidia Morocco kupata sare ya 1-1 dhidi ya Brazil katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026. (Times)
Liverpool pia wanaendelea kufanya mazungumzo kuhusu Bouaddi, huku Chelsea na Paris St-Germain wakimfuatilia mchezaji huyo ambaye anaweza kugharimu angalau £60m. (Talksport)
Bayern Munich wanaweza kukumbana na ushindani katika juhudi zao za kumsajili mshambuliaji wa PSV Eindhoven, Ismael Saibari, 25, kutokana na bao lake dhidi ya Brazil kwenye Kombe la Dunia ambalo linaweza kuongeza thamani yake. (Bild)
Beki wa Brighton, Jan Paul van Hecke, 26, amesema ataamua mustakabali wake baada ya Kombe la Dunia, kufuatia Tottenham kukataa ofa mbili zilizowasilishwa kwa ajili ya mchezaji huyo wa Uholanzi. (Sky Sports)
Manchester City wameweka macho yao kwa beki wa kati wa Everton, Jarrad Branthwaite, 23, kama mbadala wa John Stones, 32, lakini Everton wanataka £70m kwa beki huyo wa England. (Football Insider)
Roma wanajiandaa kutoa ofa ya £35m kwa kiungo mshambuliaji wa England, Mason Greenwood, 24, na kujumuisha kipengele cha mauzo ya baadaye ili kuishawishi Marseille kukubali dau hilo. (Corriere dello Sport)
Kiungo wa Brazil, Ederson, alipangwa kufanyiwa vipimo vya afya Jumapili akiwa hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United kutoka Atalanta. (Corriere dello Sport)