Je, ushawahi kusikia msemo wa Kimaasai unaosema ‘Kuchinja Dume la Nyika’?
Msemo huu ni maarufu sana katika jamii ya Kimaasai ambako maisha ya mwanaume hupitia hatua za kimila katika ukuaji.
Hatua hizo ni pamoja na kufanyiwa sherehe ya *Orkiteng le Sirit*(Kuchinjiwa Dume), ikimaanisha ni mwisho wa ujana na kuingia uzeeni.
Hapa sasa kijana huyo anaandaliwa kuingia rasmi katika maisha ya uzeeni na kuachana na tabia na makundi ya vijana.
Fuatilia video hii inayoeleza maana halisi ya ‘Dume la Nyika’.
*Imeandaliwa na Caren-Tausi Mbowe kwa msaada wa Msaada wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).
(Feed generated with FetchRSS)