• Wabunge wa jimbo la Ondo nchini Nigeria mnamo Alhamisi, Julai 25, 2019 walilazimika kukatiza vikao vyao ghafla baada ya nyoka kunyemelea bunge
  • Tukio hilo lilitokea baada ya nyoka kudondoka kutoka katika dari la jumba la bunge na wabunge kutimka bio
  • Shughuli katika bunge hilo kwa sasa zimesimamishwa hadi litakapokarabatiwa na mashimo yote yanayoweza kupitisha wanyama mfano wa nyoka kuzibwa

Wabunge wa jimbo la Ondo nchini Nigeria mnamo Alhamisi, Julai 25, walilazimika kukimbilia usalama wao baada ya nyoka wa ajabu kuzuka bungeni wakati wa kikao.

Wabunge wakanyagana wakikimbia baada ya nyoka kuanguka bungeni kutoka darini
Wabunge wa jimbo la Ondo huko Nigeria walilazimika kukatiza vikao vyao ghafla baada ya nyoka kunyemelea bunge kutokea kwenye dari. Picha: Taalabi
Source: Facebook

Tukio hilo liliwafanya wabunge wengi kuingiwa na uoga mwingi na kulazimisha vikao kusitishwa na hatimaye kuahirishwa.

Kulingaa na ripoti za vyombo vya haari nchini humo, shughuli katika bunge hilo kwa sasa zimesimamishwa hadi litakapokarabatiwa na mashimo yote yanayoweza kupitisha wanyama mfano wa nyoka kuzibwa.

“Tulipokuwa tukikaribia kuingia bungeni, nyoka mkubwa alikimbia nje ya bunge na kutufanya kuingiwa na uoga na kusababisha vikao kuahirishwa, kila mtu alikimbia” msemaji wa wabunge hao Olugbenga Omole, alisema.

Pia soma

Video ya kutisha yaonesha wakati mwanamke alipoteza maisha yake katika mchezo wa bungee jumping

Kulingana na wabunge, tukio hilo linatokea kwa sababu ya hali mbaya ya jengo la bunge ambalo linakosa pesa la kulikarabati.

Hamna aliyejeruhiwa kwenye kisa hicho, lakini mfanyakazi wa bunge alimfukuza nyoka huyo na kumpiga hadi kufa.

“Bunge sio salama na tumeamua kuahirisha vikao kwa muda ili lifanyiwe ukarabati unaofaaa na kulifanya saama kwetu,” Omule alisema.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *