Mateus Fernandes

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 2

Real Madrid imefanya mawasiliano ya awali kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa West Ham na Ureno, Mateus Fernandes, mwenye umri wa miaka 21. Hata hivyo, Manchester United bado inaonekana kuwa mbele katika mbio za kuwania saini yake. (Teamtalk)

Manchester United haiko tayari kulipa kiasi kinachotakiwa na West Ham kwa Fernandes, kinachokadiriwa kufikia pauni milioni 80. Kiungo huyo pia anawaniwa na klabu za Paris Saint-Germain pamoja na Real Madrid. (Mirror)

Bayern Munich ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Morocco, Ismael Saibari, mwenye umri wa miaka 25, kutoka PSV Eindhoven kwa ada inayozidi pauni milioni 45. (Talksport)

Real Madrid pia imeulizia uwezekan wa kumpata kiungo wa Borussia Dortmund na Ujerumani, Felix Nmecha, mwenye miaka 25. Hata hivyo, klabu yake ya zamani Manchester City pamoja na Manchester United nazo zinafuatilia uwezekano wa kumsajili. (Sky Sport Germany)

 Marcus Rashford

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Fursa na muda uliowekwa kimkataba kwa Barcelona ya kumsajili mshambuliaji wa England, Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 28, kwa euro milioni 30 (pauni milioni 35) unatarajiwa kuumalizika, bila klabu hiyo kuamua kufanya uhamisho wake wa mkopo kutoka Manchester United kuwa wa kudumu. (ESPN)

Newcastle United inatarajiwa kuongeza kasi ya mazungumzo wiki hii kwa ajili ya kumwania winga wa Osasuna na Hispania, Victor Munoz, mwenye umri wa miaka 22. (Mail)

Leeds United inapanga kufanya jaribio la kumsajili beki wa kati wa Ivory Coast, Ousmane Diomande, mwenye umri wa miaka 22, kutoka Sporting. (Football Insider)

Ipswich Town na Hull City zinaonyesha nia ya kumsajili golikipa wa England, Nick Pope, mwenye umri wa miaka 34, huku Newcastle United ikiwa tayari kumuuza kwa pauni milioni 5. (Teamtalk)

West Ham ni miongoni mwa klabu kadhaa za England zinazofuatilia kwa karibu kiwango cha winga wa Watford na Australia, Nestory Irankunda, mwenye umri wa miaka 20, katika Kombe la Dunia. (Football Insider)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *