
Viongozi wa mataifa ya G7 wanaokutana nchini Ufaransa, wanasema maelewano ya Marekani na Iran kumaliza vita Mashariki ya Kati ni fursa ya kihistoria, huku wakikubaliana pia kuendelea kuishinikiza Urusi kusitisha vita nchini Ukraine.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkutano huo wa siku tatu unaomalizika siku ya Jumatano unaongozwa na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, ambaye katika taarifa ya pamoja, ameeleza kuwa wakuu wa nchi za Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani, wamekubaliana kuhusu masuala muhimu yanayoitatiza dunia hasa kwenye suala la usalama na amani.
Viongozi hao wamesisitiza kuwa hatua ya Marekani na Iran kutarajiwa kutia saini mkataba huo wa amani siku ya Ijumaa nchini Uswizi, ni fursa ya kihistoria wakisema hatua hiyo itaizuia Theran kupata silaha za nyuklia na kuacha kutishia nchi jirani.
Aidha, imekubaliwa kuwa kikosi cha pamoja kati ya Ufaransa na Uingereza, kinaweza kuhusika pakubwa kuhakikisha kuwa shughuli za kawaida, zinarejelewa tena kwenye mlango wa baharà wa Hormuz, ili meli za mafuta na mizigo ziendelee na safari zao bila vikakwazo.
Kuhusu vita vinavyoendelea nchini Ukraine, viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuipa Kiev msaada wa silaha na kuendelea kuweka shinikizo kwa uchumi wa Urusi, ikiwemo kuongeza vikwazo kwenye sekta ya mafuta na gesi ili isitishe vita vinavyoendelea kwa mwaka wa nne sasa.