Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Safari ya Cristiano Ronaldo ya kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya sita mfululizo rekodi inayomfanya kulingana na wachezaji waliocheza mara nyingi zaidi, ilianza kwa matokeo mabaya baada ya taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Ureno katika mechi ya Kundi K iliyochezwa hapo jana Jumatano.

Bao la kichwa la Yoane Wissa kabla ya mapumziko liliwasaidia Leopards na kuipa nchi hiyo pointi yake ya kwanza kabisa katika historia ya michuano ya Kombe la Dunia.  Hii ni kabla ya bao la mapema la Jao Neves kuiweka Ureno kifua mbele. DRC, ambayo inashiriki fainali hizi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974 ilipokuwa ikijulikana kama Zaire, ilionyesha kiwango kizuri na kuhimili presha kutoka kwa Wareno.

Cristiano Ronaldo wa Ureno wakati wa mechi yao ya kombe la dunia dhidi ya Congo DR.
Cristiano Ronaldo wa Ureno wakati wa mechi yao ya kombe la dunia dhidi ya Congo DR. REUTERS – Pedro Nunes

Ronaldo mwenye umri wa miaka 41 hakung’ara sana katika mchezo huo na alishindwa kuathiri matokeo kama alivyofanya mpinzani wake wa muda mrefu Lionel Messi, ambaye siku moja kabla alikuwa amefunga mabao matatu dhidi ya Algeria.

Ureno ilianza vyema baada ya Joao Neves kufunga kwa kichwa dakika ya sita akimalizia krosi ya Pedro Neto. Hata hivyo, licha ya kumiliki mpira kwa muda mwingi, walishindwa kutumia nafasi zao vizuri.

Wachezaji wa DR Congo wakiwa na mashabiki wao baada ya mechi yao ya kombe la dunia dhidi ya Ureno.
Wachezaji wa DR Congo wakiwa na mashabiki wao baada ya mechi yao ya kombe la dunia dhidi ya Ureno. REUTERS – Annegret Hilse

Dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza, Wissa aliifungia DRC bao la kusawazisha kwa kichwa bila kuzuiwa, akimshinda kipa Diogo Costa na kuandika historia kwa kufunga bao la kwanza kabisa la nchi yake katika Kombe la Dunia.

Katika kipindi cha pili, DRC iliendelea kuonyesha ushindani mkubwa. Cedric Bakambu akikaribia kuifungia timu yake bao la ushindi lakini shuti lake liligonga mwamba wa lango huku Christiano Ronaldo pia akishindwa kuzitumia nafasi zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *