Baadhi ya vijana wanaotekeleza awamu ya pili ya programu ya ‘Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT)’ kwa upande wa sekta ya uvuvi wamesema programu hiyo imeanza kuonesha matunda baada ya samaki waliopandikizwa kwa takribani miezi 3 iliyopita kuanza kukua hadi kufikia gramu 250.
Akizungumza mmoja wa wanufaika hao Mratibu wa programu hiyo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Clemence Katunzi amesema kuwa matokeo hayo yanatokana na kujitoa kwa vijana hao kwenye huduma mbalimbali za ufugaji wa samaki hao.
Naye mnufaika, Erasto Deo ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha mikopo ya masharti nafuu isiyo na riba amesema kuwa hatua hiyo imewaonesha mwanga wa mafanikio wanayotarajia pindi watakapovuna samaki hao kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.
Mhariri @moseskwindi
(Feed generated with FetchRSS)