ARUSHA;Simba ya Dar es Salaam imetinga kibabe fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB, baada ya kuitandika Coastal Union ya Tanga mabao 4-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha muda mfupi uliopita.

Kutokana na matokeo hayo Simba sasa anasubiri mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya Yanga na Azam utakaopigwa kesho Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mabao ya Simba yamefungwa na Libasse Gueye, Nickson Kibabage, Rushine De Reuck na Clatous Chama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *