
Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan umefanyika mjini Cairo kwa ajili ya kujadili utulivu wa kikanda na kufuatilia makubaliano kati ya Iran na Marekani.
Mkutano huo umehudhuriwa na Badr Abdel Ati, Hakan Fidan, Faisal bin Farhan, na Muhammad Ishaq Dar Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Misri, Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan. Kando na mkutano huo, mkutano mwingine pia ulifanyika na Rais wa Misri. Pakistan ilitangaza kuwa mkutano huo ulifanyika ili kubadilishana maoni kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo amani, usalama, na namna ya kupanua ushirikiano.
Kulingana na Al-Arabi Al-Jadeed, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdel Ati, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Muhammad Ishaq Dar, mbali na klujadili uhusiano wa pande mbili walijadili kwa kina matukio ya kikanda hasa kadhia ya amani na usalama na makubaliano ya Iran na Marekani.
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo nne wanatarajiwa kujadili pia namna ya kuunga mkono utulivu katika eneo hilo na kufuatilia utekelezaji wa makubaliano kati ya Iran na Marekani.
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizi pia walikutana na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi pambizoni mwa mkutano huo.
Mkutano wa mwisho wa pamoja wa mawaziri wa mambo ya nje wa Pakistan, Misri, Saudi Arabia, na Uturuki ulifanyika mwishoni mwa Aprili 2024 katika pambizoni mwa Jukwaa la Diplomasia la Antalya, huku mkutano wake wa kwanza ukiandaliwa na Islamabad mnamo tarehe 9 Machi 2024.