Mkuu wa Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga Gilbert Kalima ameupokea mwenge wa uhuru kwaajili ya kuukimbiza katika Wilaya hiyo ukiwa Matika Wilaya ya Tanga ambapo Mkuu wa Wilaya ya Tanga amemkabidhi mwenge huo leo Juni 22.06.2027
Katika Wilaya hiyo Mwenge wa Uhuru utatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.8 ambapo ni pamoja na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi minne ikiwemo miwili ya elimu, jengo la OPD na mradi wa uchakataji wa mazao ya Mkonge sambamba na kuzindua mradi mmoja wa maji utakaosaidia kukabili adha ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, na kukagua mradi wa Kikundi cha Vijana wanaolima Mwani.
(Feed generated with FetchRSS)