Weekend iliyopita mwanadada African Princess Nandy The African Princess ameanza safari ya tamasha lake kubwa la Nandy Festival 2026, safari hii akianzia mkoani Shinyanga katika viwanja vya ShyCom ambapo mashabiki wameonyesha muitikio mkubwa.
Licha ya matamasha mengi ya muziki kuacha kufanyika nchini, mwanadada Nandy ameendelea kusimama imara na kuonyesha mafanikio makubwa katika tasnia hiyo kupitia tamasha lake hilo.
Tamasha hilo limewakutanisha katika stage moja Nandy, Rayvanny, Billnass, Linah, Pipi Jojo,Bando Mc, Mon Centralzone, Stamina, Gnako, Mullaobo na Kuss Love ambao kwa ujumla wametoa burudani ya kiwango cha juu.
Pongezi kwa Nandy kwa uthubutu wake wa kuendelea kuwekeza kwenye matamasha na kuonyesha kwamba bado kuna nafasi kubwa ya mafanikio katika tasnia ya burudani Tanzania.
✍️✍️ victor
🎥🎥 The African Princess
The African Princess Faustina Charles Nandy Festival 2026 NENGA MAFIOSO CHUI… 🐯
(Feed generated with FetchRSS)