Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametangaza kusitishwa kwa vikwazo vya mafuta na kuondolewa kwa mzingiro wa majini

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ameripoti kuwa marufuku ya mauzo ya mafuta na bidhaa za petrokemikali nje ya nchi imesitishwa, huku mzingiro wa majini ukiondolewa.

Aidha, Araghchi amesema kuwa baadhi ya mali za Iran zilizokuwa zimezuiwa nje ya nchi zimeachiwa, na kwamba mpango mkubwa wa Iran wa ujenzi upya wa uchumi na maendeleo umeanza kutekelezwa.

Waziri huyo alitangaza hayo kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X.

Pia aliishukuru Pakistan na Qatar kwa juhudi zao za upatanishi, akisema kuwa mazungumzo hayo “yameleta maendeleo makubwa katika kumaliza vita nchini Lebanon.”

Araghchi alikuwa akirejelea vifungu vya 1, 10 na 11 vya hati ya makubaliano ya maelewano kati ya Iran na Marekani, ambavyo utekelezaji wake ndio msingi wa mazungumzo yanayoendelea kuelekea kufikiwa kwa makubaliano ya mwisho.

Kifungu cha 1 kinasema kuwa Marekani, Iran na washirika wao watatangaza kusitishwa mara moja na kwa kudumu kwa operesheni za kijeshi katika maeneo yote ya mzozo, ikiwemo Lebanon.

Kifungu cha 10 kinahusu utoaji wa vibali na misamaha inayohitajika kwa usafirishaji wa mafuta, bidhaa za petroli na huduma zinazohusiana nazo, ikiwemo sekta za benki na usafiri.

Kifungu cha 11 kinahusu mali za Iran zilizozuiwa nje ya nchi, suala ambalo lilikuwa miongoni mwa vikwazo vikubwa katika mazungumzo hayo.

Kwa sasa, Araghchi yuko nchini Uswisi kwa ajili ya duru ya mazungumzo yanayoendelea kati ya Iran na Marekani kuhusu makubaliano ya mwisho ya kumaliza mzozo na kupunguza mvutano wa kikanda.

#chanzoBBCSWAHILI
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *