
Dar es Salaam. Bunge la Tanzania leo Jumanne, Juni 23, 2026 limeipitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Sh62.3 trilioni ya mwaka 2026/27 kwa kura 385 sawa na asilimia 97 ya kura zote 393.
Akitangaza matokeo, Spika wa Bunge, Mussa Zungu amesema jumla ya kura zilizopigwa 385 na wabunge wanane hawakuwapo bungeni, huku kura za hapana zikiwa nane.
Bajeti hiyo iliwasilishwa bungeni Juni 11, 2026 na Waziri wa Fedha, Balozi Khamisi Mussa Omar. Ilijadiliwa kwa siku saba za kazi kuanzia Juni 15 hadi leo Jumanne, ilipohitimishwa kwa Balozi Omar na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mukumbo kujibu hoja mbalimbali zilizoibuka wakati wa mjadala huo.
Aidha, Spika wa Bunge, Mussa Zungu ameitaka Serikali kwenda kusimamia ipasavyo Bajeti Kuu ya Serikali ya Sh62.3 trioni inatumika kwa maslahi ya wananchi na siyo vinginevyo huku akisisitiza, Bunge litakuwa linafuatilia.
Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Ilala (CCM) amesema hayo leo baada ya Bunge kuipitisha bajeti hiyo kwa kura 385 kati ya 393 zilizopigwa sawa na asilimia 97.
Endelea kufuatilia Mwananchi…