Dar es Salaam. Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa WhatsApp wasiopenda kuungwa kwenye makundi bila ridhaa zao wakumbuke wanaweza kuzuia kuwekwa kwenye makundi hayo kupitia sehemu ya mipangilio (settings).

Mtumiaji anatakiwa kwenda kwenye settings, kuchagua Privacy, kisha Groups. Hapo ataweza kuchagua ni nani anayeruhusiwa kukuweka kwenye group.

Miongoni mwa chaguo zilizopo ni Everyone (kila mtu), My Contacts (watu waliopo kwenye orodha ya mawasiliano) au My Contacts Except… ambapo mtumiaji anaweza kuchagua watu wasioweza kumuongeza kwenye makundi.

Hatua hizo zinalenga kuimarisha faragha, kupunguza usumbufu wa kuongezwa kwenye makundi yasiyotakiwa na kusaidia watumiaji kutumia data kwa ufanisi zaidi wanapotumia huduma za WhatsApp.

Jinsi ya kupunguza matumizi ya Mb ukipiga simu WhatsApp

Katika hatua nyingine mtandao huo umekuja na kipengele kinachowapa watumiaji udhibiti zaidi wa matumizi ya data na faragha zao.

Kwa watumiaji wanaotumia huduma ya simu za sauti au video kupitia WhatsApp, wanaweza kupunguza matumizi ya intaneti kwa kuwasha kipengele cha Use Less Data for Calls.

Ili kufanya hivyo, mtumiaji anatakiwa kwenda kwenye sehemu ya Settings, kisha Storage and Data, na kuwasha chaguo la Use Less Data for Calls.

Kipengele hicho hupunguza kiwango cha data kinachotumika wakati wa mawasiliano ya sauti au video, jambo linalosaidia hasa kwa watumiaji wenye vifurushi vidogo vya intaneti au wanaotumia mtandao wenye kasi ndogo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *