Marekani imesitisha rasmi vikwazo vyake dhidi ya mafuta ya Iran siku ya Jumatatu hadi Agosti 21, kama sehemu ya makubaliano yaliyosainiwa na Tehran.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limesababisha bei ya mafuta kushuka, ambayo tayari ilikuwa ikishuka. Bei ya pipa la mafuta ghafi ya Brent kutoka Bahari ya Kaskazini, kiwango cha kimataifa, ilikuwa ikiuzwa kwa karibu dola 77.80 saa 8:00 mchana jana Jumatatu.

“Miamala yote” ambayo hapo awali ilikuwa “imepigwa marufuku” kuhusu uzalishaji, uuzaji, na usafirishaji wa hidrokaboni zenye asili ya Iran “imeidhinishwa hadi Agosti 21 saa 6:01 usiku” saa za Washington, kulingana na leseni iliyochapishwa kwenye tovuti ya Wizara ya Hazina ya Marekani, ambayo inasimamia vikwazo vya kiuchumi.

Hatua hii imechukuliwa baada ya Washington kusema kuwa Iran iko tayari kuwaruhusu tena wakaguzi wa shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya atomiki IAEA kuitembelea nchi hiyo.

Kumeripotiwa pia hali ya utulivu katika mapigano nchini Lebanon chini ya makubaliano hayo yanayolenga kukomesha uhasama katika eneo lote la Mashariki ya Kati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *