
Marekani siku ya Jumatatu imeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu “dalili za kutisha kwamba ukatili mkubwa unaweza kufanyika” huko El-Obeid, mji mkuu nchini Sudan ambapo Umoja wa Mataifa pia unahofia kutokea kwa shambulio la wanamgambo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika taarifa, Wizara ya Mambo ya Nje ilizitaka pande zinazopigana “kukomesha kitendo chochote kinachoweza kuhatarisha maiasha ya raia, kuzuia misaada ya kibinadamu, au kuchangia katika ukatili zaidi.”
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilielezea wasiwasi wake mkubwa siku ya Jumamosi huku “idadi kubwa ya wanajeshi” wakikusanyika kuzunguka mji huo.
El-Obeid, katika eneo la Kordofan, imekuwa ikizingirwa kwa miezi kadhaa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), ambavyo vimekuwa vikipigana na jeshi la serikali tangu mwezi Aprili 2023.
Wiki iliyopita, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Sudan alimpigia simu kamanda wa RSF, Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, kumwomba asishambulie El-Obeid na kusisitiza “hitaji la haraka la kupunguza hali hiyo.”
“Hatupaswi kuruhusu vitisho vya El-Fasher kurudiwa El-Obeid,” alisisitiza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.
Vikosi vya RSF vinashutumiwa kwa kufanya ukatili mwingi wakati wa kukamatwa kwa mji wa El-Fasher mwezi Oktoba, jiji kubwa la mwisho huko Darfur ambalo bado linaendelea kuonysha upinzai wao dhidi ya wanamgambo hao. Mnamo mwezi Februari, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta ukweli hata uliripoti vitendo vya “mauaji ya kimbari.”
Tangu kuanguka kwa jiji hili mikononi mwa wanamgambo wa RSF, mapigano yameongezeka, haswa katika eneo la Kordofan, mapigano makali yanayohusisha ngome za SRF huko Darfur na maeneo yanayodhibitiwa na jeshi mashariki mwa Sudan.