Dar es Salaam. Msanii akiondoka kwenye lebo kubwa ya muziki mara nyingi huonekana kama anaenda kupotea kwenye gemu. Hatahivyo hilo ni tofauti kwa Mbosso ambaye safari yake kama msanii huru imejaa mafanikio.

Tangu aachane na WCB, Mbosso amekuwa akiachia kazi mfululizo zenye mapokezi makubwa sokoni. Miongoni mwa nyimbo hizo Pawa, Aviola, Ozalima, Sipo Single na DJ. Ambazo zimeendelea kufanya vizuri katika vituo vya redio, majukwaa ya kuuzia muziki na mitandao ya kijamii.

Katika kipindi cha takribani mwaka mmoja, kazi zake zimeonekana kuimarisha zaidi uwepo wake kwenye soko la muziki wa Afrika Mashariki. 

Mbali na kazi zake binafsi, pia ameshirikiana na wasanii wakubwa kama Harmonize pamoja na Alikiba. Hatua inayotajwa kuongeza mvuto na ushawishi kwenye gemu.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za majukwaa ya muziki. Mbosso alitajwa kuwa miongoni mwa wasanii waliotafutwa zaidi nchini Tanzania kwenye Boomplay mnamo Juni 19, 2026. Huku kwenye Audiomack akirekodi zaidi ya mara milioni 129 za kusikilizwa (plays), ishara ya ukuaji wa kasi wa muziki wake baada ya kuanza safari ya kujitegemea.

Nyimbo kama Ozalima, Pawa na Darasa la Saba zimeendelea kubeba uzito mkubwa katika orodha ya kazi zake zinazofanya vizuri, zikimpa nafasi ya kudumisha mashabiki wake wa zamani huku akivutia wapya.

Kutokana na mwendelezo huu wa mafanikio, unaonesha kuwa Mbosso ameweza kujisimamia mwenyewe na kuendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika Bongo Fleva. Hatua inayomuweka kuwa miongoni mwa wasanii wanaofuatiliwa kwa karibu zaidi katika kizazi hiki cha muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *