Polisi dawati la jinsia na watoto wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza limetoa onyo kwa wazazi wanaowatelekeza watoto ambao baadhi yao ufanyiwa vitendo vya ukatili.
Onyo hili limetolewa jijini Mwanza na mkuu wa dawati la jinsia na watoto wilaya ya Nyamagana mrakibu msaidizi wa polisi Pill Sabuli Heriel.
Mkuu huyo wa dawati la jinsia pia ameihasa jamii kutoa taarifa za vitendo vya ukatili ili watakaobainika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wake mkuu wa kituo cha polisi Nyakato mrakibu wa polisi Prisca Sarabanze amewakumbusha wazazi wazingatie malezi bora ya familia huku mkuu wa dawati la jinsia akisisitiza kwamba huduma bora inatolewa kwa watu wa lika zote.
Dawati la jinsia wilaya ya Nyamagana linaendelea kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili kwa makundi mbalimbali.
(Feed generated with FetchRSS)