Kombe la Dunia la FIFA 2026 limeandika historia kwa kuwa mashindano yenye mahudhurio makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa, baada ya kuvunja rekodi iliyokuwa imedumu tangu mwaka 1994.
FIFA imethibitisha kuwa hadi Juni 25, jumla ya mashabiki 3,605,357 walikuwa tayari wameingia viwanjani kushuhudia mechi za Kombe la Dunia 2026, na hivyo kupita rekodi ya awali ya mashabiki 3,587,538 iliyowekwa kwenye Kombe la Dunia la 1994 nchini Marekani.
Rekodi hiyo ilitangazwa wakati wa mchezo kati ya Ecuador na Ujerumani, huku viwanja vikijaa kwa wastani wa zaidi ya asilimia 99 ya uwezo wake. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi kwani mashindano bado yanaendelea kuelekea hatua za mtoano.
Mafanikio hayo yanaonyesha jinsi Kombe la Dunia la 2026, linalofanyika kwa mara ya kwanza katika nchi tatu za Marekani, Canada na Mexico pamoja na kushirikisha timu 48, lilivyozidi kuvutia mashabiki kutoka sehemu mbalimbali duniani.

(Feed generated with FetchRSS)