
Baadhi ya mechi za hatua ya 32 ya Kombe la Dunia 2026 zimeanza kujulikana zikikutanisha timu zilizofanya vizuri katika hatua ya makundi.
Hadi leo Ijumaa, Juni 26, 2026, kuna mechi nne za hatua ya 32 ambazo tayari zimeshafahamika zitakutanisha timu zipi.
Mchezo ambao hadi sasa unaonekana utakuwa wa msisimko ni utakaozikutanisha Morocco na Uholanzi ambao utachezwa nchini Mexico katika Uwanja wa Montrerrey.
Morocco imefuzu hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kushika nafasi ya pili kwenye kundi C wakati Uholanzi imeingia katika hatua hiyo baada ya kuongoza kundi F.
Mechi hiyo itachezwaJuni 30, 2026 kuanzia saa 10:00 alfajiri kwa muda wa Afrika Mashariki.
Wenyeji Canada wao watakutana na Afrika Kusini katika mechi itakayochezwa Juni 28, 2026 katika Uwanja wa SoFi.
Juni 29 kutakuwa na mechi nyingine ya hatua ya 32 bora ambayo itazikutanisha Brazil na Japan.
Wenyeji Marekani watakutana na Bosnia&Herzegovina katika mechi itakayochezwa Julai 2, 2026.