Kazem Gharibabadi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisheria na Kimataifa amesisitiza kuwa, Tehran itafuatilia kwa uzito jukumu la wahusika wa uhalifu wa mashambulio ya mabomu ya kemikali yaliyofanywa na utawala wa zamani wa Iraq.

Gharibabadi amesema hayo katika ujuumbe wake katika mtandao wa kijamii kwa manasaba wa kumbukumbu ya miaka 39 ya mashambulio ya mabomu ya kemikali dhidi ya mji wa Sardasht ulioko magharibi mwa Iran.

Aidha amesema, mji wa Sardasht haukuwa mwathirika tu wa mabomu ya kemikali; lakini pia ulikuwa mwathirika wa undumakuwili na kimya cha nchi kama Ujerumani, Marekani, Uingereza na Uholanzi, ambazo ziliipatia serikali ya Saddam silaha hizi zisizo za kibinadamu na kisha kuzifumbia macho mateso ya maelfu ya waathiriwa. Tunafuatilia kwa uzito jukumu la wahusika wa uhalifu huu.

Miaka 39 iliyopita katika siku kama ya leo mji wa Sardasht huko magharibi mwa Iran ulishambuliwa kwa mabomu ya kemikali na ndege za kivita za utawala wa zamani wa Iraq. Raia wasio na ulinzi 110 wa Iran wakazi wa mji huo waliuawa shahidi na wengine 530 kujeruhiwa katika mashambulizi hayo ya utawala wa zamani wa Saddam Hussein. Utawala wa Saddam ambao ulikuwa umekata tamaa ya kupata ushindi katika medani za vita dhidi ya Iran ulikuwa ukidhani kwamba kwa kufanya mashambulizi hayo ya kemikali dhidi ya raia wa mji wa Sardasht ungeweza kulitwisha taifa la Iran matakwa yake. Taasisi muhimu za kimataifa na madola makubwa duniani hata hivyo hazikuchukua hatua yoyote ya jadi ya kuuzuia utawala wa Saddam kutumia silaha za kemikali wala hata kulaani jinai hizo ulizozifanya dhidi ya raia wasio na hatia wa Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *