
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, utoaji wa huduma za “kiufundi na usaidizi” kwa pande zinazoshambulia kuwa ni jukumu la moja kwa moja na la wazi katika kupigana vita haramu vya hiari na kama ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.
Akijibu kauli za maafisa wa Italia walioona ushiriki wa nchi hiyo katika vita vya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran kuwa mdogo kwa “msaada wa kiufundi na vifaa” na kwa hivyo wakakataa kuwa na ushirikiano wowote katika vita dhidi ya Iran, Ismail Baghaei ameandika kwenye ukurasa wake binafsi:
Huu ni mgongano na hila dhahiri inayolenga kukwepa jukumu la kushiriki katika kosa kubwa la kimataifa: kwa upande mmoja, unakataa hadharani msaada wowote au usaidizi kwa wavamizi, lakini wakati huo huo unasema kwamba ulitoa huduma za “kiufundi na usaidizi” kwa wahusika wa uvamizi; huduma zilizowezesha vita haramu vya uvamizi vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa: “Kutoa huduma za “kiufundi na usaidizi” kwa wahusika wa uchokozi kwa kweli si kitu kingine zaidi ya kuwa na jukumu la moja kwa moja na la waziwazi katika vita haramu, kitendo cha wazi cha uchokozi, na ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.
Hivi karibuni pia msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisisitiza kwamba, Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) na nchi wanachama wake, zikiwemo Italia na Romania, ambazo Katibu Mkuu wa NATO amekiri waziwazi nafasi yao katika kutekeleza mashambulizi haramu na ya kihalifu dhidi ya Iran, zinapaswa kuwajibishwa kwa aina yoyote ya ushirikiano katika uhalifu uliofanywa na Marekani na Israel dhidi ya Iran.