Baada ya Ujerumani kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2026, kipa wa timu hiyo, Manuel Neuer ametangaza kustaafu soka la kimataifa.

Katika mchezo huo wa jana dhidi ya Paraguay, Ujerumani ilipoteza kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya mechi baina ya timu hizo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 katika dakika 120 za kawaida.

Neuer, ambaye alizaliwa upya na kurejea kikosini kwa ombi maalum la kocha Julian Nagelsmann kwa ajili ya mashindano hayo, amehitimisha sura yake ya mwisho akiwa na jezi ya timu ya taifa kwa masikitiko baada ya ndoto zake kukwama mapema kuliko ilivyotarajiwa.

Licha ya matokeo hayo machungu, hakuna anayeweza kufuta ukweli kwamba Neuer anaondoka uwanjani kama mmoja wa makipa bora zaidi kuwahi kutokea katika historia ya soka duniani.

Alikuwa nguzo muhimili ya mafanikio ya Ujerumani, ikiwemo ubingwa wa Kombe la Dunia wa mwaka 2014 nchini Brazil.

“Ni maumivu makubwa sana kumaliza katika namna hii. Tulikuwa na kila kitu mikononi mwetu.

“Na ninaamini kwamba tuna wachezaji sahihi wa kukamilisha hilo vizuri ndani ya uwanja. Lakini kama timu, tumeshindwa kucheza soka vyema,” amesema Neuer.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *