KUNA taarifa za mshambuliaji wa JKT Tanzania, Paul Peter kuhitajika na klabu ya Al Ahly Benghazi, ili kumsajili kwa ajili ya msimu ujao, baada ya kufanya vizuri msimu uliomalizika.
Chanzo kutoka Libya kilisema, timu hiyo imepeleka ofa kwa uongozi wa nyota huyo, ambao bado wanaichambua kama inaweza ikawa na manufaa kwa mchezaji huyo, licha ya kuwa fursa kwenda kupata chalenji mpya nje lakini wanaweka mbele maslahi.
Peter mwenye miaka 27, amemaliza msimu akiwa na mabao tisa, asisti tatu na alikuwa na kiwango cha juu. Huo ni muendelezo wa kiwango alichokionyesha katika misimu miwili aliyokuwa Dodoma Jiji akifunga mabao 11.
Chanzo kutoka Libya kilisema: “Kuna mawakala ambao wanafuatilia wachezaji kutoka nchini mbalimbali ikiwemo Tanzania ambayo kwa sasa soka lake lipo juu, miongoni mwa hao ni Peter ambaye kiwango chake kimekuwa kikubwa.”
Alipotafutwa mchezaji huyo ili kuthibitisha kinachoendelea kuhusishwa na Al Ahly Benghazi, amesema: “Natambua kuna ofa kama nilivyoambiwa na meneja wangu, lakini bado hatujakaa na kuzungumza kwani ndiyo kwanza tumetoka kumaliza msimu wa Ligi Kuu Bara.