Nchini Iran, kuanzia leo shughuli za mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa kiroho Ayatollah Ali Khamenei, zimeanza kuelekea kuzikwa kwake, baada ya kuuawa kwenye vita dhidi ya nchi yake na Marekani Pamoja na Israel miezi kadhaa iliyopita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mwili wake umewasimi kwenye ukumbi mkubwa wa dini ya Kiislamu wa Mosalla jijini Tehran.

Maombolezo yataendelea Jumamosi katika jiji Kuu Tehran na yanatarajiwa kuendelea na kumaliza Julai 9, wakati Ayatolla Ali Khamenei, atakapozikwa nyumbani kwake katika mji wa Mashhad, Kaskazini Mashariki mwa Iran.

Watu zaidi ya Milioni 20 wanatarjiwa jijini Tehran kushiriki kwenye maombolezo hayo.

Wakati hayo yakijiri, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Iran Esmaeil Baghaei, ameishtumu Marekani kwa kuendelea kuonesha nia ya kweli kuhakikisha kuwa amani ya kudumu inapatikana.

Iran na Marekani licha ya kusaini mkataba wa kumaliza vita, suala la usimamizi wa eneo la mlango wa Bahari ya Hormuz, mradi wa nyuklia na kuendelea kuzuia fedha za Tehran ni miongoni mwa masuala tata yanayoendelea kujadiliwa ili kupata mkataba wa kudumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *