Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya kituo cha utafiti kuhusu idadi ya watu na afya barani Afrika, inaonesha kuwa maelfu ya wanawake nchini Kenya wanaendelea kupoteza maisha kwa sababu ya utoaji mimba usiokuwa salama.

Shirika hilo linakadiria kuwa mwaka 2023, kulikuwa na visa vya 793,000 vya utaoaji mimba, huku 300,000 wakitoa mimba kila mwaka.

Aidha, utafiti umebaini kuwa wanawake wapatao 2,600 walipoteza maisha kwa utoaji mimba usio salama mwaka 2023.

Daktari Samson Mwita aliyeshiriki kwenye utafiti huo, amesema kituo chake cha afya hupokea mabinti na wanawake kati ya 60 na 90 kila mwezi wenye matatizo yanayotokana na utoaji mimba.

Utoaji mimba nchini Kenya ni kinyume cha sheria, japo utoaji mimba unaruhusiwa tu pale maisha ya mama yanapokuwa hatarini.

Kwa mujibu wa sheria za Kenya, kosa la utoaji au kushiriki kwenye utoaji mimba, adhabu yake ni kati ya miaka 3-14 jela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *