Chanzo cha picha, Getty Image
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2
Manchester United inajiandaa kuwasilisha ofa kwa ajili ya kiungo wa Brighton, Carlos Baleba, mwenye umri wa miaka 22, raia wa Cameroon, baada ya kushindwa kumsajili Mateus Fernandes. (Give Me Sport)
Arsenal bado ina dhamira ya kumsajili kiungo wa Newcastle United, Bruno Guimaraes, mwenye umri wa miaka 28, na inaandaa ofa ikiamini kuwa dau la pauni milioni 60 linaweza kukamilisha uhamisho wa Mbrazili huyo. (The Sun)
Huku mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez akihusishwa na uhamisho kwenda Barcelona, Atletico Madrid imemtaja aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United, Mason Greenwood, mwenye umri wa miaka 24 na anayekipiga Marseille, kuwa mbadala wake. (Sport – Spain)
Kipa wa Arsenal, Kepa Arrizabalaga, mwenye umri wa miaka 31, ameiambia klabu hiyo kuwa anataka kuondoka msimu huu wa joto, huku kipa wa zamani wa Leeds United, Illan Meslier, mwenye umri wa miaka 26, akitajwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kuchukua nafasi yake. (Teamtalk)
Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal pia inaonyesha nia ya kumsajili beki wa Aston Villa na timu ya taifa ya England, Ezri Konsa, mwenye umri wa miaka 28, katika dirisha hili la usajili. (The Telegraph)
Mshambuliaji wa Aston Villa na England, Ollie Watkins, mwenye umri wa miaka 30, anasakwa na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki. (The Sun)
Leeds United imewasilisha ofa iliyoboreshwa ya pauni milioni 23 pamoja na nyongeza kwa ajili ya kiungo wa Southampton, Shea Charles, mwenye umri wa miaka 22, baada ya ofa yao ya awali kukataliwa. (Daily Mail)
AC Milan inapanga kumuuza beki wa England, Fikayo Tomori, mwenye umri wa miaka 28, msimu huu wa joto huku akielekea mwaka wa mwisho wa mkataba wake. (Gazzetta dello Sport)
Kiungo wa Roma na Morocco, Neil El Aynaoui, mwenye umri wa miaka 25, anafuatiliwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu England, zikiwemo Manchester United, Liverpool, Chelsea, Aston Villa, Brighton, Bournemouth, Newcastle United na Sunderland. (Teamtalk)
Everton ni klabu ya hivi karibuni ya Ligi Kuu England kuhusishwa na kiungo wa Benfica na Colombia, Richard Rios, mwenye umri wa miaka 26, ambaye anawindwa na vilabu kadhaa. (Sport Witness)