Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umetangaza fursa za uwekezaji katika viwanja 38 vinavyomilikiwa na Serikali vilivyopo katika mikoa 20, vitakavyoendelezwa kupitia ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP).
Kupitia tangazo la kuonesha nia ya uwekezaji (Expression of Interest – EOI), TBA imesema miradi hiyo inahusisha makazi, biashara, matumizi mchanganyiko, vituo vya ugavi na usafirishaji, pamoja na hoteli na utalii.
Miongoni mwa maeneo yaliyotangazwa ni ekari 630 za Nzuguni jijini Dodoma, pamoja na viwanja vya Masaki, Oysterbay, Magomeni na Pugu jijini Dar es Salaam, huku maeneo mengine yakipatikana Arusha, Mwanza, Mbeya, Morogoro, Kigoma, Geita, Tabora, Kagera, Songwe na mikoa mingine.
TBA imesema miradi hiyo itatekelezwa kupitia mfumo wa PPP kufuatia kupanuliwa kwa majukumu yake mwaka 2023, na inatarajiwa kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi, kuongeza ajira na kuharakisha maendeleo ya sekta ya majengo nchini.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)