Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imesema Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, Sabasaba, yamechangia kuzalishwa kwa ajira zaidi ya 631,109 katika kipindi cha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Pamoja na ajira zote hizo, inatarajia zaidi ya ajira 20,000 zitapatikana kupitia maonesho ya mwaka huu.

Akizungumza katika ufunguzi rasmi wa maonesho hayo jijini Dar es Salaam mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Dkt. Latifa Khamis, amesema maonesho hayo yameendelea kuwa chachu ya biashara, uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Amesema katika kipindi cha miaka 50, Sabasaba imekuwa jukwaa la kuunganisha wazalishaji, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, hatua iliyochochea fursa za ajira na maendeleo ya sekta mbalimbali za uchumi.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *