Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesema umeanza mchakato wa kuchakata nyaraka za watumishi wanaotarajiwa kustaafu katika mwaka wa fedha 2026/2027, hatua inayolenga kuhakikisha wanalipwa mafao yao kwa wakati mara wanapohitimisha utumishi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea banda la PSSSF katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Fortunatus Magambo amesema wanaendelea kuhakiki na kuhuisha taarifa za wanachama mapema ili kurahisisha uchakataji wa mafao wanapofikia umri wa kustaafu.

Alisema uwezo wa PSSSF kulipa mafao kwa wakati umeimarika kufuatia kuongezeka kwa ukwasi wa Mfuko baada ya Serikali kulipa deni la muda mrefu la michango ya wanachama lililokuwa likiidai PSSSF.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *