Vyombo vya habari kama vile mashirika ya habari, vituo vya televisheni na magazeti ya kimataifa vimeonyesha umuhimu mkubwa kwa hafla ya mazishi ya Imam shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, ambapo tukio hilo limewekwa katika nafasi ya juu ya habari za kimataifa kwa kuripotiwa kwa karibu na kwa kina.

Vvyombo vya habari vya kigeni vimeangazia kwa mapana ana amarefu mazishi na utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa kiongozi shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran. Sambamba na kuanza kwa mazishi ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mjini Tehran, vyombo vya habari vya nje vilichapisha ripoti za moja kwa moja, picha, video na uchambuzi mbalimbali, vikiakisi tukio hilo kwa upana mkubwa na kuliweka katika nafasi ya juu ya habari zake za kimataifa.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa, hafla rasmi za mazishi ya mwili wa kiongozi shahidi wa Mapinduzi zimeanza na zitadumu kwa siku kadhaa. Ripoti hiyo pia imeeleza kuwepo kwa idadi kubwa ya maafisa wa serikali na viongozi kutoka mataifa ya nje waliohudhuria katika hafla hiyo.

Baadhi ya Vyombo vya habari vya China vimeeleza kwamba, hafla hii ya mazishi ni alama ya umoja na nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, huku baadhi yao zikizitaja kuwa ni miongoni mwa matukio muhimu zaidi ya kisiasa na kidini katika eneo hili kwa mwaka huu.

Aidha, Reuters imefafanua mipango na maandalizi yaliyofanywa na Iran ili kuandaa mazishi yenye heshima kubwa ya kumuaga Imam shahidi, ikiwa ni pamoja na hatua za kiusalama, kiitifaki na za kiutawala zilizoratibiwa kwa ajili ya tukio hilo muhimu.

Vyombo vya habari vya Uturuki, ikiwemo Shirika la Habari la Anadolu, kituo cha TRT, magazeti ya kitaifa na vyombo vya habari vya mtandaoni, vimeeleza kuwa mazishi ya Imam shahidi ni miongoni mwa matukio muhimu zaidi ya kisiasa na kidiplomasia katika eneo. Vyombo hivyo vimeweka mkazo maalum kwenye uwepo wa marais wa nchi mbalimbali na wajumbe wa ngazi ya juu waliohudhuria.

Pia, sehemu kubwa ya uchambuzi uliotolewa na vyombo vya habari vya Uturuki umejikita katika athari za kikanda za tukio hilo, mustakabali wa uhusiano wa Iran na nchi jirani, pamoja na mchango wake katika mabadiliko yanayoendelea katika Mashariki ya Kati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *