
Mamilioni ya watu leo wamejitokeza katika Musalla wa Imam Khomeini mjini Tehran na kutoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi Shahidi Imam Khamenei aliyeuawa shahidi Februari 28 mwaka huu katika mashambulio ya kinyama ya Marekani na utawala haramuu wa Israel.
Wakiwa na nyuso za huzuni, ghamu na masikitiko makubwa, waombolezaji hao wakiwa wamevaa mavazi meusi kama ishara ya simanzi kwa tukio chungu la kuondokewa na kiongozi wao walibubujikwa na machozi na kuaangua vilio.
Wakati huo huo vyombo rasmi vya habari vya Kamati ya Maandalizi ya mazishi ya Kiongozi wa Shahidi wa Mapinduzi vimetangaza kuwa Swala ya maiti ya Imam Mujahid shahidi pamoja na familia yake itaswaliwa saa 6:00 asubuhi ya kesho, Jumapili, katika Musalla wa Imam Khomeini hapa mjini Tehran.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa maandalizi ya usalama na ratiba ya hafla hiyo yamekamilika, huku mamlaka zikitarajia ushiriki mkubwa wa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Wakati huo huo, viongozi waandamizi wa Iran, marais na wakuu wa nchi, pamoja na wageni mashuhuri na wajumbe wa ngazi za juu kutoka mataifa mbalimbali duniani, wamefika Tehran kutoa buriani na heshima zao za mwisho kwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.
Katika hafla iliyojaa uzito wa kihistoria na maombolezo, iliyofanyika Ijumaa katika Ukumbi wa Sala wa Tehran (Musalla), wakuu wa mihimili mitatu ya utawala Iran, serikali kuu, bunge na mahakama, wakiongozana na marais, maspika wa mabunge, wajumbe maalum, wanazuoni, wasomi wa dini na wanafikra kutoka pembe mbalimbali za dunia, walihudhuria hafla ya kutoa heshima kwa Shahidi Ayatullah Khamenei.